Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 3:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithubutisha hakiya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu aletae ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibin-Adamu.)

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Lakini, ikiwa uovu wetu unathibitisha kwamba Mungu anatenda kwa haki, tutasema nini? Je, tutasema kwamba anakosa haki akituadhibu? (Hapa naongea kibinadamu).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Lakini, ikiwa uovu wetu unathibitisha kwamba Mungu anatenda kwa haki, tutasema nini? Je, tutasema kwamba anakosa haki akituadhibu? (Hapa naongea kibinadamu).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Lakini, ikiwa uovu wetu unathibitisha kwamba Mungu anatenda kwa haki, tutasema nini? Je, tutasema kwamba anakosa haki akituadhibu? (Hapa naongea kibinadamu).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Lakini ikiwa uovu wetu unathibitisha haki ya Mungu waziwazi, tuseme nini basi? Je, Mungu kuileta ghadhabu yake juu yetu ni kwamba yeye si mwenye haki? (Nanena kibinadamu.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ikiwa uovu wetu unathibitisha haki ya Mungu waziwazi, tuseme nini basi? Je, Mungu kuileta ghadhabu yake juu yetu ni kwamba yeye si mwenye haki? (Nanena kibinadamu.)

Tazama sura Nakili




Waroma 3:5
32 Marejeleo ya Msalaba  

Msijilipize kisasi, wapenzi, bali ipisheni ghadhabu; maana imeandikwa, Kisasi juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.


bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,


Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:


Kwa maana, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kwa sababu ya uwongo wangu hatta akapata utukufu, mbona mimi nami ningali nikihukumiwa kama ni mwenye dhambi?


BASSI, tusemeje? Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili amepata nini?


Bali Mungu aonyesha pendo lake kwetu, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.


TUSEME nini bass? Tudumu katika dhambi illi neema iwe nyingi zaidi?


Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa maana kama mlivyotoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na maasi mpate kuasi, vivyo sasa toeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.


Tusemeje, bassi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalijua dhambi illa kwa sharia: kwa maana singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.


Bassi, na tuseme nini baada ya hayo? Mungu akiwa upande wetu, nani aliye juu yetu?


Tuseme nini, bassi? Ya kwamba watu wa mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; yaani ile haki iliyo ya imani;


Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na nyama wakali kule Efeso, nina faida gani wasipofufuka wafu? Tule, tukanywe, maana kesho tutakufa.


Je! ninanena haya kama mwana Adamu? Au sharia nayo haisemi yayo hayo?


bali katika killa neno tukijipatia sifa njema, kama wakhudumu wa Mungu, katika saburi nyingi, kalika mateso, katika shidda, katika taabu,


Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele za Mungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na khofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi. Kwa killa njia mmejionyesha kuwa safi katika jambo hilo.


Maana nikiyajenga tena yale niliyoyabomoa, naonyesha ya kuwa mimi mwenyewe ui mkosaji.


Ndugu, nanena kwa jiusi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwana Adamu, illakini likiisha kuthuimtika, hapana mtu alibatilishae, wala kuliongeza neno.


Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.


Furahini juu yake, enyi mbingu, na ninyi watakatifu na mitume na manabii, kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo