Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 3:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 Bassi, je! twaibatilisha sharia kwa imani hiyo? Hasha! kinyume cha hayo twaithubutisha sharia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Je, tunaitumia imani kuibatilisha sheria? Hata kidogo; bali tunaipa sheria thamani yake kamili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Je, tunaitumia imani kuibatilisha sheria? Hata kidogo; bali tunaipa sheria thamani yake kamili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Je, tunaitumia imani kuibatilisha sheria? Hata kidogo; bali tunaipa sheria thamani yake kamili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Je, basi ni kwamba tunaibatilisha sheria kwa imani hii? La, hasha! Badala yake tunaithibitisha sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Je, basi ni kwamba tunaibatilisha sheria kwa imani hii? La, hasha! Badala yake tunaithibitisha sheria.

Tazama sura Nakili




Waroma 3:31
27 Marejeleo ya Msalaba  

Mkalitangua neno la Mungu kwa mapokeo yemi.


Yesu akajibu, akamwambia, Hayo yaache sasa: kwa kuwa hivi imetupasa kutimiza haki yote. Bassi akamwacha.


Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.


Maana nawaambieni, Haki yenu isipozidi kuliko haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.


Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.


Kwa maana Kristo ni mwisho wa sharia, illi killa aaminiye apate haki.


mkufunzi wra wajiuga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati,


Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na killa mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Illi upewe haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.


Hasha! kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?


Maana ikiwa wale wa sharia ndio warithi, imani imekuwa burre, na ahadi imebatilika.


Kwa maana naifurahia sharia ya Mungu kwa mtu wa ndani,


Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Bassi, kama ni hivi, kwa akili zangu naitumikia sharia ya Mungu, bali kwa mwili sharia ya dhambi.


illi wema uagizwao na torati utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.


Kwa wale wasio na sharia nalikuwa kama sina sharia. Si kana kwamba sina sharia mbele za Mungu, hali mwenye sharia mbele za Kristo, illi niwapate wasio na sharia.


Maana mimi kwa sharia naliifia sharia illi nimwishie Mungu.


Siibatili neema ya Munga. Maana, ikiwa haki hupatikana kwa sharia, bassi, Kristo alikufa burre.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo