Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 3:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 kama tukijali kwamba Mungu ni mmoja, atakaewapa wale waliotahiriwa haki itokayo katika imani, nao wasiotahiriwa liaki kwa njia ya imani hiyo hiyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Mungu ni mmoja, naye atawafanya Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Mungu ni mmoja, naye atawafanya Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Mungu ni mmoja, naye atawafanya Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Basi kwa kuwa kuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani hiyo hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Basi kwa kuwa tuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani iyo hiyo.

Tazama sura Nakili




Waroma 3:30
18 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi ikiwti yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! kutokutahiriwa kwake hakutahesahiwa kuwa kutahiriwa?


Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?


ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.


Bassi, twahasibu ya kuwa mwana Adamu hupewa baki kwa imani pasipo matendo ya sharia.


Kwa hiyo ilitoka kwa imani, iwe kwa njia ya neema, illi ile ahadi iwe imara kwa wazao wote, si kwa wale wa torati tu, illa na kwa wale wa imani ya Ibrahimu aliye baba yetu sisi sote,


Bassi ukheri huu ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba Ibrahimu kwa ajili ya imani yake aliliesabiwa wema.


Aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


Na andiko, likiona tangu zamani kwamba Mungu atawafanyizia mataifa wema kwa imani, lilimkhubiri Ibrahimu Injili zamani, ya kama, Kwa wewe mataifa yote yatabarikiwa.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili.


Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wana Adamu ni mmoja, mwana Adamu, Kristo Yesu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo