Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 3:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Bassi, twahasibu ya kuwa mwana Adamu hupewa baki kwa imani pasipo matendo ya sharia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Maana Mungu humkubali mtu kuwa mwadilifu kwa imani, wala si kwa kutimiza matakwa ya sheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Maana Mungu humkubali mtu kuwa mwadilifu kwa imani, wala si kwa kutimiza matakwa ya sheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Maana Mungu humkubali mtu kuwa mwadilifu kwa imani, wala si kwa kutimiza matakwa ya sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Kwa maana twaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kupitia kwa imani wala si kwa matendo ya sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Kwa maana twaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa matendo ya sheria.

Tazama sura Nakili




Waroma 3:28
20 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


illi aonyeshe haki yake wakati huu, awe mwenye baki na mwenye kumpa haki yeye aaminiye kwa Yesu.


Lakini kwa mtu asiofanya kazi, bali anamwammi yeye ampae haki asiye mtawa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.


Na hivyo sharia imekuwa mwalimu wa kutuleta kwa Kristo, illi tufanyiziwe wema kwa imani.


Na andiko, likiona tangu zamani kwamba Mungu atawafanyizia mataifa wema kwa imani, lilimkhubiri Ibrahimu Injili zamani, ya kama, Kwa wewe mataifa yote yatabarikiwa.


wala si kwa matendo, asije mtu awae yote akajisifu.


tena nionekane katika yeye, nisiwe na baki ile ipatikanayo kwa sharia, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;


tukifanyiziwa wema kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.


Lakini mtu atasema, Wewe una imani, nami nina matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo yako, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.


Lakini wataka kujua, wewe mwana Adamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?


Mwaona kwamba mwana Adamu ahesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa iinaui peke yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo