Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 3:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Maana hapana tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, wanaona kwamba wamepungukiwii utukufu wa Mungu:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Watu wote wametenda dhambi na wametindikiwa utukufu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Watu wote wametenda dhambi na wametindikiwa utukufu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Watu wote wametenda dhambi na wametindikiwa utukufu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,

Tazama sura Nakili




Waroma 3:23
17 Marejeleo ya Msalaba  

Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wuyafanye yasiyowapasa;


Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi illi awarehemu wote.


Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:


Ni nini bassi? Tu bora kuliko wengine? Hatta kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba wote pia wa chini ya dhambi;


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.


illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.


aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, illi kuupata ntukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.


BASSI, ikiwa ikaliko abadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.


lakini kama mnavyoyashiriki mateso va Kristo furahini; illi na katika ufimuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.


NAWASIHI wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadae;


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo