Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 3:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Kwafaa sana kwa killa njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Naam, iko faida kwa kila upande. Kwanza, Mungu aliwakabidhi Wayahudi ujumbe wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Naam, iko faida kwa kila upande. Kwanza, Mungu aliwakabidhi Wayahudi ujumbe wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Naam, iko faida kwa kila upande. Kwanza, Mungu aliwakabidhi Wayahudi ujumbe wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa maneno halisi ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile Neno halisi la Mungu.

Tazama sura Nakili




Waroma 3:2
29 Marejeleo ya Msalaba  

Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:


Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema nae katika mlima Sinai, tena pamoja na baba zetu: ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.


ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu,


na kuyajua mapenzi yake na kuyatambua manibo yaliyo bora, umeelimishwa katika torati,


BASSI Myahudi ana ziada gani? na kutahiriwa kwafaa nini?


Ni nini, bassi, ikiwa hawakuamini wengine? Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?


ambao ni Waisraeli, wenye kufanywa wana, wenye utukufu na maagano, wenye kupewa torati na ibada ya Mungu na ahadi zake; ambao mababu ni wao,


Maana nikiitenda kazi hii kwa khiari yangu nina thawabu; kama si kwa khiari yangu, illakini nimeaminiwa uwakili.


yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; nae ametia ndani yetu neno la upatanisho.


bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili va wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa


Timotheo, ilinde amana, ukijiepisha na maneno yasiyo ya dini, yasiyo maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa nwongo;


Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita) mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Akaniambia, Haya ni maneno ya uaminifu na ya kweli. Na Bwana Mungu wa manabii watakatifu alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake mambo ambayo hayana buddi kuwa upesi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo