Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 2:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, hasira na ghadhabu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Lakini kwa wale wanaotafuta mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

Tazama sura Nakili




Waroma 2:8
34 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ghadhahu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wana Adamu waipingao kweli kwa uovu wao.


Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu?


Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yanga, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu,


Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;


Bassi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kujulisha uweza wake kwa uvumilivu mwingi alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;


Lakini mtu aliye yote, akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.


Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;


ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, nzushi,


na hawa wengine kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa illi niitetee Injili.


Msitende neno lo lote kwa kushindana na kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, killa mtu na amhesabu mwenziwe kuwa hora kuliko nafsi yake;


katika mwako wa moto, akiwalipa kisasi wao wasiomjua Mungu, nao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Maswali ya upuzi, na vitabu vya nasaba, na magomvi, na mashindano ya sharia, ujiepushe nayo. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.


bali kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.


Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, akatoka aende hatta mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na magomvi mioyoni mwenu msijisifu, wala msiseme nwongo juu ya kweli.


maana hapo palipo wivu na magomvi, ndipo palipo machafuko, na killa tendo la aibu.


KADHALIKA ninyi wake, watumikieni waume o zenu; kusudi, ikiwa wako waume wasioliamini Neno, kwa mwenendo wa wake zao, pasipo Neno lile, wavutwe;


Kwa maana wakati umefika hukumu ianzie nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu, nini mwisho wao wasioitu Injili ya Mungu?


yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.


Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo