Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 2:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Bassi ikiwti yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! kutokutahiriwa kwake hakutahesahiwa kuwa kutahiriwa?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Kama mtu wa mataifa mengine ambaye hakutahiriwa akitimiza matakwa ya sheria, hakika atafikiriwa kana kwamba ametahiriwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Kama mtu wa mataifa mengine ambaye hakutahiriwa akitimiza matakwa ya sheria, hakika atafikiriwa kana kwamba ametahiriwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Kama mtu wa mataifa mengine ambaye hakutahiriwa akitimiza matakwa ya sheria, hakika atafikiriwa kana kwamba ametahiriwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Hivyo, ikiwa wale wasiotahiriwa wanatimiza mambo ambayo Torati inataka, je, kutokutahiriwa kwao hakutahesabiwa kuwa sawa na kutahiriwa?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Hivyo, ikiwa wale wasiotahiriwa wanatimiza mambo ambayo sheria inataka, je, kutokutahiriwa kwao hakutahesabiwa kuwa sawa na kutahiriwa?

Tazama sura Nakili




Waroma 2:26
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Ee mwanamke, imani yako kubwa; pata utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.


Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sharia, lakini ukiwa mvunjaji wa sharia kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.


Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?


kama tukijali kwamba Mungu ni mmoja, atakaewapa wale waliotahiriwa haki itokayo katika imani, nao wasiotahiriwa liaki kwa njia ya imani hiyo hiyo.


illi wema uagizwao na torati utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.


Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.


Kwa ajili ya hayo kumbukeni kwamba zamani, ninyi mlio watu wa mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa jina lenu wasiotahiriwra na wale wanaoitwa jina lao waliotahiriwa, yaani tohara ya mwili kwa mikono:


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili.


Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mkono, kwa kuuvua mwili wa dhambi, wa nyama, kwa tohara ya Kristo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo