Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 2:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wana Adamu, sawa sawa na injili yangu, kwa Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kupitia kwa Isa Al-Masihi, kama isemavyo Injili yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Isa Al-Masihi, kama isemavyo Injili yangu.

Tazama sura Nakili




Waroma 2:16
31 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Kwa maana hakuna neno lililostirika ambalo halitakuwa dhabiri, wala neno lililofichwa ambalo halitajulikana, na kutokea wazi.


Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.


Akatuagiza tuwakhubiri watu na kushuhudu ya kuwa huyu udiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa hayi na wafu.


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,


Hasha! kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?


NAWAARIFU, ndugu, injili niliyowakhubirieni; ndiyo mliyoipokea, katika hiyo mnasimama,


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya.


Kwa maana injili biyo niliyowakhubiri nawajulisha, ndugu, ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.


kama vile ilivyonenwa katika injili ya utukufu wa Mungu ahimidiwae, niliyoaminiwa mimi.


Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daud, kama inenavyo injili yangu.


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


Na jinsi watu wanavyowekewa kufa marra moja, na baada ya kufa hukumu:


watakaotoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hayi na waliokufa.


Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo