Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 2:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na wakishitakiana killa mtu mwenzake kwa fikara zao na kuteteana;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Wao wanaonesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Wao wanaonyesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea.)

Tazama sura Nakili




Waroma 2:15
18 Marejeleo ya Msalaba  

Nao, waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianza tangu wazee hatta wa mwisho; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke akisimama katikati.


PAOLO akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa nia safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hatta leo hivi.


Nami ninajizoeza katika neno hili kuwa na dhamiri isiyo na khatiya mbele ya Mungu na mbele ya watu.


Kwa maana watu wa mataifu wasio na sharia wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, bao wasio na sharia wamekuwa sharia kwa nafsi zao wenyewe:


Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?


NASEMA kweli katika Yesu Kristo, sisemi uwongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu,


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


Bassi tukiijua khofu ya Bwana, twawavuta wana Adamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tunadhihirishwa katika dhamiri zenu pia.


kwa unafiki wa watu wasemao uwongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;


Vitu vyote ni sali kwao walio safi: lakini hapana kilicho safi kwa walio najis, wasioamini, bali akili zao na nia zao pia zimekuwa najis.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo