Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 2:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Kwa sababu sio waisikiao torati walio wenye haki mbele ya Mungu, bali ni wale waitendao torati watakaohesabiwa kuwa wenye haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa maana si wale wanaoisikia sheria ambao ni wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaohesabiwa haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa maana si wale wanaoisikia sheria ambao ni wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaohesabiwa haki.

Tazama sura Nakili




Waroma 2:13
29 Marejeleo ya Msalaba  

Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.


Lakini yeye akajibu akawaambia, Mama yangu na ndugu zangu ndio hawa walisikialo neno la Mungu na kulitenda.


Mkiyajua hayo, m kheri mkiyatenda.


na kwa huyu killa amwaminiye huhesabiwa kuwa hana khatiya katika mambo yale asiyoweza kuhesabiwa kuwa hana khatiya kwa torati ya Musa.


Kwa maana Musa aieleza haki itokayo kwa sharia, akiandika ya kuwa, Mtu afanyae haya ataishi kwa haya.


Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sharia, lakini ukiwa mvunjaji wa sharia kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.


kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia.


Maana hapana tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, wanaona kwamba wamepungukiwii utukufu wa Mungu:


kama tukijali kwamba Mungu ni mmoja, atakaewapa wale waliotahiriwa haki itokayo katika imani, nao wasiotahiriwa liaki kwa njia ya imani hiyo hiyo.


Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabikiwi haki kwa ajili hiyo; illa aninukumuye ni Bwana.


tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.


Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kufanyiziwa wema kwa sharia; mmeanguka toka hali ya neema.


Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.


Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyae haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo