Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 2:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sharia watapotea pasipo sharia, na wote waliokosa, wakiwa na sharia, watahukumiwa kwa sharia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Wale wanaotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Wale wanaotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Wale wanaotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Watu wote waliotenda dhambi pasipo sheria wataangamia pasipo sheria, nao wote waliotenda dhambi chini ya sheria watahukumiwa kwa sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Watu wote waliotenda dhambi pasipo sheria wataangamia pasipo sheria, nao wote wale waliotenda dhambi chini ya sheria watahukumiwa kwa sheria.

Tazama sura Nakili




Waroma 2:12
23 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini, nawaambieni, itakuwa rakhisi Turo na Sidon istahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.


Lakini nawaambieni, itakuwa rakhisi inchi ya Sodom istahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.


Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.


mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua:


ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao haya wamestahili mauti, wanafanya haya, wala si hivyotu, bali wakubaliana nao wayatendao.


Kwa sababu sharia ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipo sharia, hapana kosa.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Kwa wale wasio na sharia nalikuwa kama sina sharia. Si kana kwamba sina sharia mbele za Mungu, hali mwenye sharia mbele za Kristo, illi niwapate wasio na sharia.


Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye.


Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.


Maana mtu awae yote atakaeishika sharia yote, na pamoja na hayo, akijikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo