Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 16:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 nisalimieni kanisa lililomo katika nyumba yao. Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Salimuni pia kundi la waumini wanaokutana nyumbani mwao. Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Al-Masihi huko jimbo la Asia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Lisalimuni pia kundi la waumini linalokutana nyumbani mwao. Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Al-Masihi huko Asia.

Tazama sura Nakili




Waroma 16:5
20 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa wawili au watatu walipo wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.


Wakapita katika inchi ya Frugia na Galatia, wakakatazwa na Roho Mtakatifu, wasilikhubiri Neno katika Asia.


Hatta Gallio alipokuwa Prokonsuli wa Akaya, Wayahudi wakamwendea Paolo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu,


Na alipotaka kuvuka bahari aende hatta Akaya, ndugu wakamhimiza, wakamwandikia barua kwa wanafunzi wale wamkaribishe; nae alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu.


Waparthi na Wamedi na Waelamiti, nao wakaao Mesopotamia, Yahudi ua Kappadokia, Ponto na Asia,


Tʼena malimbuko yakiwa matakatifu, vivyo hivyo na, donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo vivyo hivyo.


maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu katika Yerusalemi walio maskini.


Nisalimieni Trufina na Trufosa, wenye ijtihadi katika Kristo.


waliokuwa tayari hatta kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, illa na makanisa ya mataifa yote pia;


Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yetu.


Nisalimieni Amplia, mpenzi wangu katika Bwana.


Tena nawasihi, ndugu, (mnaijua nyumba ya Stefano kwamba ni malimbuko ya Akaia, nao wamejitia katika kazi ya kuwakhudumu watakatifu),


Makanisa ya Asia wawasalimu. Akula na Priskilla wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililo ndani ya nyumba yao.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia:


Maana najua utajiri wenu, niliojisifia kwa Wamakedoni, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo watu wengi.


Wasalimuni ndugu walio katika Laodikia, na Numfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.


na kwa Appia, ndugu yetu mpendwa, na kwa Arkippo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako;


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


MZEE kwa Gaio mpenzi, nimpendae katika kweli.


Hawa udio wasiotiwa najis pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana kondoo killa aendako. Hawa walinunuliwa katika inchi, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo