Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 15:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Bassi nasema, Yesu Kristo amefanyika mkhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithubutishe ahadi walizopewa haha zetu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kwa maana nawaambia kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonesha kweli ya Mungu, na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kwa maana nawaambia kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu, na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani,

Tazama sura Nakili




Waroma 15:8
29 Marejeleo ya Msalaba  

Nae akajibu, akasema, Sikupelekwa illa kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli.


kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.


Alikuja kwake, nao walio wake hawakumpokea.


Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja.


Paolo na Barnaba wakanena kwa uthabiti wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza: illakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, wala hamjioni nafsi zenu kuwa mmestahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia mataifa.


Fahamu, bassi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka ukali, bali kwako wema, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.


Kwa maana kama ninyi zamani mlimwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kutokuamini kwao,


illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.


illi aonyeshe haki yake wakati huu, awe mwenye baki na mwenye kumpa haki yeye aaminiye kwa Yesu.


Ni nini, bassi, ikiwa hawakuamini wengine? Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?


Kwa hiyo ilitoka kwa imani, iwe kwa njia ya neema, illi ile ahadi iwe imara kwa wazao wote, si kwa wale wa torati tu, illa na kwa wale wa imani ya Ibrahimu aliye baba yetu sisi sote,


Bassi, nasema neno hili, ya kwamba killa mtu wa kwenu husema, Mimi wa Paolo, na mimi wa Apollo, na mimi wa Kefa, na mimi wa Kristo.


Bassi niseme nini? ya kwamba sanamu ni kitu? au ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu?


Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?


Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika.


Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; na katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa kazi yetu.


kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo