Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 15:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Kwa hiyo mkaribishane, kama nae Kristo alivyotukaribisha, illi Mungu atukuzwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Basi, karibishaneni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo alivyowakaribisheni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Basi, karibishaneni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo alivyowakaribisheni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Basi, karibishaneni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo alivyowakaribisheni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Karibishaneni ninyi kwa ninyi kama Al-Masihi alivyowakaribisha ninyi ili kumletea Mungu utukufu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Karibishaneni ninyi kwa ninyi kama Al-Masihi alivyowakaribisha ninyi ili kumletea Mungu utukufu.

Tazama sura Nakili




Waroma 15:7
15 Marejeleo ya Msalaba  

Awapokeae ninyi, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenituma.


Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma.


Mafarisayo na wandishi wakanungʼunika, wakasema, Huyu hukaribisha wenye dhambi, hula pamoja nao.


akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa.


Amri mpya nawapeni, mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, na ninyi mpendane vivyo hivyo.


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


nao Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa sababu hii nitakusifu katika Mataifa, Na jina lako nitaliimba.


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


illi sisi tuwe sifa ya utukufu wake, tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu;


macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,


mkichukuliana, na kuachiliana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mtu; jinsi Kristo alivyowaachilieni, vivyo hivyo na ninyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo