Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 15:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Nakusihini, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami kwa maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo uletwao na Roho, mniunge mkono kwa kuniombea kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo uletwao na Roho, mniunge mkono kwa kuniombea kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo uletwao na Roho, mniunge mkono kwa kuniombea kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi na kwa upendo wa Roho wa Mungu, kujiunga nami katika taabu zangu mkiniombea kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi na kwa upendo wa Roho wa Mwenyezi Mungu, kujiunga nami katika taabu zangu mkiniombea kwa Mungu.

Tazama sura Nakili




Waroma 15:30
16 Marejeleo ya Msalaba  

ninyi nanyi mkisaidiana kwa ajili yetu katika kuomba, illi, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa kazi ya watu wengi, watu wengi watoe mashukuru kwa ajili yetu.


Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na maumivu, na dhiiki, na adha, na shidda, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo ua nguvu.


Maana sisi tulio hayi siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, illi uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ipatwayo na manti.


Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


na mimi pia, nipewe usemi, kwa kufumhua kinywa changu kwa ujasiri, niikhubiri siri ya Injili,


BASSI ikiwako faraja iliyo yote katika Kristo, yakiwako ma, tulizo yo yote ya mapenzi, ikiwako huruma yo yote na rehema,


nae alitueleza upendo wenu katika Roho.


MAANA nataka muijue juhudi niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili, jinsi ilivyo kuu;


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


ILIYOBAKI, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, likatunzwe vilevile kama ilivyo kwenu;


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo