Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 15:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yanga, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Sithubutu kusema kitu kingine chochote isipokuwa tu kile ambacho Kristo Yesu amekifanya kwa kunitumia mimi ili watu wa mataifa wapate kutii. Amefanya hivyo kwa maneno na vitendo,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Sithubutu kusema kitu kingine chochote isipokuwa tu kile ambacho Kristo Yesu amekifanya kwa kunitumia mimi ili watu wa mataifa wapate kutii. Amefanya hivyo kwa maneno na vitendo,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Sithubutu kusema kitu kingine chochote isipokuwa tu kile ambacho Kristo Yesu amekifanya kwa kunitumia mimi ili watu wa mataifa wapate kutii. Amefanya hivyo kwa maneno na vitendo,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa maana sitathubutu kusema kitu chochote zaidi ya kile ambacho Al-Masihi amefanya kwa kunitumia mimi katika kuwaongoza watu wa Mataifa wamtii Mungu kwa yale niliyosema na kufanya,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa maana sitathubutu kusema kitu chochote zaidi ya kile ambacho Al-Masihi amefanya kwa kunitumia mimi katika kuwaongoza watu wa Mataifa wamtii Mungu kwa yale niliyosema na kufanya,

Tazama sura Nakili




Waroma 15:18
28 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi yule aliyepokea talanta tano akashika njia, akafanya kazi nazo, akachuma talanta nyingine tano.


Nao wakatoka, wakakhubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithubutishia neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Amin.


Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.


Bassi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paolo wakiwapasha khabari za ishara na maajabu ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika mataifa.


Walipofika Yerusalemi wakakaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.


Na baada ya kuwasalimu, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyotenda katika mataifa kwa khuduma yake.


hali kwanza niliwakhubiri wale wa Dameski na Yerusalemi, na katika inchi yote ya Yahudi, na watu wa mataifa, watubu wakamwelekee Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;


Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;


Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliye mtukufu hatta milele, ajua va kuwa sisemi nwongo.


Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini nitajizuia, mtu asinihesabie zaidi ya haya ayaonayo kwangu au kuyasikiakwa kinywa changu.


si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu,


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


(maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha kwenda kwa mataifa);


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema.


Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, akatoka aende hatta mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


Mwe watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, mkijidanganya nafsi zenu.


Watoto, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, biali kwa tendo na kweli.


Lakini Mikael, malaika mkuu, aliposhindana na Shetani, na kuhujiana nae kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana akukemee.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo