Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 15:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Na mimi mwenyewe, ndugu zangu, nimehakikishwa kwa khahari zenu kama ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba nyinyi pia mmejaa wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana nyinyi kwa nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba nyinyi pia mmejaa wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana nyinyi kwa nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba nyinyi pia mmejaa wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana nyinyi kwa nyinyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Ndugu zangu, mimi mwenyewe ninasadiki kwamba mmejaa wema, mkijazwa ufahamu wote na mnaweza kufundishana ninyi kwa ninyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Ndugu zangu, mimi mwenyewe ninasadiki kwamba mmejaa wema na ufahamu wote, tena mnaweza kufundishana ninyi kwa ninyi.

Tazama sura Nakili




Waroma 15:14
25 Marejeleo ya Msalaba  

kwa kuwa katika killa jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote;


Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, ipendavyo Roho yule yule;


Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi.


NA kwa khabari ya vitu, vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna elimu. Elimu huleta majivuno, bali upendo hujenga.


Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na elimu, umeketi chakulani ndani ya hekalu ya sanamu, je! dhamiri yake mtu huyu, kwa kuwa yu dhaifu, haitathubutika hatta ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?


Bali elimu hii haimo ndani ya watu wote; illa wengine kwa kuizoelea ile sanamu hatta sasa hula kama ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri yao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika.


Lakini kama mlivyo na wingi wa vitu vyote, imani, na matamko, na elimu, na bidii yote, na mapenzi yenu kwetu sisi; bassi vivyo hivyo mwe na wingi wa neema hii pia.


(kwa kuwa tunda la nura ni katika wema wote na haki na kweli);


mmejazwa matuuda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.


kama ilivyo wajib wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kuitetea Injili na kuithubutisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii.


Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.


Bassi, farijianeni mkajengeane, killa mtu mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, illi Mungu wetu awahesabu kuwa nimeustahili wito wenu, akatimize killa haja ya wema na killa kazi ya imani kwa nguvu:


nikikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, iliyokaa kwanza katika bibi yako Loi, na katika mama yako Euniki; aa ninasadiki ya kwamba na wewe nawe unayo.


Nikiamini kutii kwako nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.


Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita) mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.


Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika khabari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokofu:


Kwa hiyo sitakosa kuwakumbusheni hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthubutishwa katika kweli iliyowatikia.


Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamwijui kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uwongo wo wote utokao katika kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo