Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 14:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Bassi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali mtoe hukumu hii, ndugu asitiwe kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu au kumsababisha aanguke katika dhambi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu au kumsababisha aanguke katika dhambi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu au kumsababisha aanguke katika dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana. Badala yake mtu aamue kutoweka kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine.

Tazama sura Nakili




Waroma 14:13
26 Marejeleo ya Msalaba  

Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u chukizo kwangu: maana huyawazi mambo ya Mungu, bali yaliyo ya wana Adamu.


Ole wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana buddi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletae jambo la kukosesha!


MSIHUKUMU, illi msihukumiwe


Na mbona ninyi katika nafsi zenu hamwamui yaliyo haki?


Ingemfaa huyu zaidi jiwe la kusagia litiwe shingoni pake akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa hawa wadogo.


Na Daud asema, Meza yao iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;


Lakini wewe je! mbona wamhukumu ndugu yako? na wewe je! mbona wamdbarau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.


Yeye alae asimdharau yeye asiyekula, nae asiyekula asimhukumu yeye alae; kwa maana Mungu amemkubali.


Wewe u nani unaemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, maana Bwana aweza kumsimamisha.


Nawasihini, ndugu, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.


Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunaui wala Kanisa la Mungu:


Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu. Je! inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa chake?


Maana upendo wa Kristo watulazimisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba ikiwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, bassi walikufa wote;


Tusiwe kwao la namna yo yote katika jambo lo lote, khuduma yetu isilaumiwe;


mpate kuyakubali yaliyo mema; illi mwe na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo,


Bassi napenda wajane wasio wazee waolewe, wazae watoto, watawale mambo ya nyumbani, wasimpe adui nafasi ya kulaumu;


je! hamkufanya ihtilafu mioyoni mwenu mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?


Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu.


Yeye ampendae ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.


Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaam, yeye aliyemfundisha Balak atie ukwazo mbele ya wana wa Israeli, wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo