Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 14:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 LAKINI yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, illakini msimhukumu mawazo yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mkaribisheni yeye ambaye imani yake ni dhaifu, lakini si kwa kugombana na kubishana juu ya mawazo yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Mkaribisheni yeye ambaye imani yake ni dhaifu, lakini si kwa kugombana na kubishana juu ya mawazo yake.

Tazama sura Nakili




Waroma 14:1
31 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala kitani kitokacho moshi hatakizima, Hatta aletapo hukumu yake ikashinda.


Marra Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?


Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.


kwa sababu hakimwingii moyoni, illa tumboni tu; kiisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.


Ingemfaa huyu zaidi jiwe la kusagia litiwe shingoni pake akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa hawa wadogo.


Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka.


Washenzi wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana walikoka moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyokunywa na kwa sababu ya baridi.


Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhayi baada ya kufa?


Mtu mmoja ana imani, anakula vyote, lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.


Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno ambalo ndugu yako hukwazwa au kuangushwa au kuwa dhaifu.


Yeye alae asimdharau yeye asiyekula, nae asiyekula asimhukumu yeye alae; kwa maana Mungu amemkubali.


BASSI imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza nafsi zetu.


Kwa hiyo mkaribishane, kama nae Kristo alivyotukaribisha, illi Mungu atukuzwe.


Asiyekuwa dhaifu wa imani, wala hakutia moyoni hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa (akiwa amekwisha kupata miaka mia), wala hali ya kufa ya tumbo lake Sara.


Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, illi niwapate wanyonge. Nalikuwa mtu wa hali zote kwa watu wote, illi nipate kuwaokoa watu kwa njia zote.


Mpokeeni, bassi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Lakini chakula kigumu in cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.


Mtu akija kwenu, nae haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo