Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 13:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru: astahiliye khofu, khofu; astahiliye heshima, heshima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Mlipeni kila mtu kile mnachodaiwa. Kama mnadaiwa kodi lipeni kodi, kama ni ushuru, lipeni ushuru, astahiliye hofu, mhofu, astahiliye heshima, mheshimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Mlipeni kila mtu kile mnachodaiwa. Kama mnadaiwa kodi lipeni kodi, kama ni ushuru, lipeni ushuru, astahiliye hofu, mhofu, astahiliye heshima, mheshimu.

Tazama sura Nakili




Waroma 13:7
23 Marejeleo ya Msalaba  

Akanena, Hutoa. Nae alipoingia nyumbani, Yesu akatangulia kumwuliza, akinena, Waonaje, Simon? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? kwa wana wao au kwa wageni?


Wakamwambia, Ya Kaisari. Akawaambia, Bassi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.


Wakamwambia, Ya Kaisari. Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. Wakamtaajahia sana.


Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo?


Akawaambia, Bassi, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.


Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona mtu huyu amipotosha taifa letu, anawakataza watu wasimpe Kaisari kodi, akisema ya kwamba yeye mwenyewe yu Kristo, mfalme.


Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;


Kwa sababu hiyo tena mwatoa kodi; kwa kuwa wao ni watumishi wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyohiyo.


Illakini killa mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; na mke asikose kumstahi mumewe.


Watumwa, watiini walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili kana kwamba ni kumtii Kristo, kwa khofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo,


Na pamoja na hayo wajifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi, hujishughulisha na mambo ya wengine wakinena maneno yasiyowapasa.


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


WO wote waiio chini ya mafungo, hali ya utumwa, wawahesabu bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.


Ninyi wanme kadhalika, kaeni na wake zenu kwa akili; mkimpa mke heshima, kama chombo kisieho nguvu, na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi sala zenu zisizuiliwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo