Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 13:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Na hayo, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia: kwa maana sasa wokofu u karibu yetu kuliko tulipoamini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Zaidi ya hayo, nyinyi mnajua tumo katika wakati gani: Sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu uko karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Zaidi ya hayo, nyinyi mnajua tumo katika wakati gani: Sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu uko karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Zaidi ya hayo, nyinyi mnajua tumo katika wakati gani: sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu uko karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Nanyi fanyeni hivi, mkiutambua wakati tulio nao. Saa ya kuamka kutoka usingizini imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu umekaribia kuliko hapo kwanza tulipoamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Nanyi fanyeni hivi, mkiutambua wakati tulio nao. Saa ya kuamka kutoka usingizini imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu umekaribia zaidi kuliko hapo kwanza tulipoamini.

Tazama sura Nakili




Waroma 13:11
25 Marejeleo ya Msalaba  

Na assubuhi, Leo dhoruba; kwa maana uwingu ni mwekundu, na kumetanda. Enyi wanafiki, mnajua kuutamhua uso wa uwingu; hali ishara za zamani hizi hamziwezi.


Bassi hayo yaanzapo kuwa, tazameni juu, mkainue vichwa vyenu kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.


Haya yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa illi kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.


Erevukeui kama ipasavyo, wala insiteude dhambi; kwa maana wengine hawamfahamu Mungu. Ninasema haya niwafedheheshe.


Kwa biyo anena, Amka, wewe usinziae, kafufuka, na Kristo atakuangaza.


Bassi, na ninyi subirini, jithubutisheni mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.


Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala:


Bassi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na ntawa,


Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wahesabuvyo kukawia, bali huvumilia kwenu, hapendi mtu aliye yote apotee, bali wote wafikilie toba.


Watoto, ni wakati wa mwisho: na kama vile mlivyosikia kwamba adui wa Kristo yuaja, hatta sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.


Yu kheri asomae, nao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyafanya yaliyoandikwa humo: maana wakati ni karibu.


Akaniambia, Msiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.


Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa killa mtu kama itakavyokuwa kazi yake.


Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo