Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 12:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 ikiwa khuduma, tuwemo katika khuduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. Mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. Mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. Mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kama ni kuhudumu na tuhudumu, mwenye kufundisha na afundishe,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kama ni kuhudumu na tuhudumu, mwenye kufundisha na afundishe,

Tazama sura Nakili




Waroma 12:7
31 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul.


ya kuwa sikuficha neno lo lote liwezaio kuwafaeni, bali naliwaonyesha na kuwafundisha kwa wazi na nyumba kwa nyumba,


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku.


Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.


Pana tofauti za khuduma, na Bwana vule yule;


Imekuwaje bassi, ndugu? Mkutanapo pamoja, killa mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana lugha, ana ufunuo, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.


Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.


Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu,


Mwambieni Arkippo, Iangalie sana khuduma ile uliyopewa katika Bwana, illi uitimize.


kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.


Bassi imempasa askofu kuwa mtu asiyelaumiwa, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, mfundishaji;


Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao.


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.


Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezae kufundisha, mvumilivu,


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo