Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 12:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Bassi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kadiri ya neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kadiri ya neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kadiri ya neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Tuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Tuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani.

Tazama sura Nakili




Waroma 12:6
31 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji;


Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili: tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.


Na kwa hiyo hekima ya Mungu ilisema, Nitatuma kwao manabii na mitume, na wataua baadhi yao, na kuwaudhi,


NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul.


Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha.


Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, Nitawamwagia watu wote Roho yangu, Na wana wenu na binti zenu watatabiri, Na vijana wenu wataona maono: Na wazee wenu wataota ndoto:


Mtu huyu alikuwa na binti wane, mabikira, waliotabiri.


kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapeni karama ya rohoni, illi mfanywe imara;


Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia killa mtu alioko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyoamgawi killa mtu kadiri ya imani.


Bali Mungu amevitia viungo killa kimoja katika mwili kama alivyotaka.


Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi.


UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu.


Lakini wote wakikhutubu, akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, alaumiwa na wote, ahukumiwa na wote;


Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapamhanue.


Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.


Maana nipendalo ni watu wote wawe kama mimi nilivyo; illakini killa mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.


Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.


ambayo hawakujulishwa wana Adamu katika vizazi vingine, jinsi walivyofunuliwa zamani hizi mitume wake watakatifu na manabii katika Roho;


Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu,


Bassi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hatta mkiwaza mengine katika lo lote, Mungu atawafunulieni hilo nalo.


Mkijua neno hili ya kwamba hapana unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fullani tu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo