Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 12:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Msijilipize kisasi, wapenzi, bali ipisheni ghadhabu; maana imeandikwa, Kisasi juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana Mwenyezi.

Tazama sura Nakili




Waroma 12:19
24 Marejeleo ya Msalaba  

bali mimi nawaambieni, Msishindane na mtu mwovu; bali mtu akupigae shavu la kuume, mgeuzie na la pili.


Wabarikini wanaowafukuzeni; barikini, wala msilaani.


Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Andaeni yaliyo mema machoni pa watu wote.


Fanya mema, utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga burre: ni mtumishi wa Mungu, amlipizae kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.


wala msimpe nafasi Shetani.


mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana.


Iskander mfua shaba alinionya mabaya mengi; Bwana atamlipa kwa jinsi ya matendo yake.


Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo