Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 12:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine.

Tazama sura Nakili




Waroma 12:10
30 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini kwemi ninyi haitakuwa hivi: bali ye yote atakae kuwa mkuu kwenu, na awe mkhudumu wenu;


Walakini ukiitwa, enenda ukaketi pahali pa chini: illi akija yeye aliyekuita akuamhie, Rafiki yangu, jongea huku mbele; ndipo utakapokuwa na heshima machoni pao wote waketio pamoja nawe.


Haya nawaamuru, mpate kupendana.


Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


Na jamii ya watu walioamini walikuwa moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.


Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru: astahiliye khofu, khofu; astahiliye heshima, heshima.


Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Msitende neno lo lote kwa kushindana na kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, killa mtu na amhesabu mwenziwe kuwa hora kuliko nafsi yake;


tuliposikia khabari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;


Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Heshimuni walu wote. Upendeni udugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema.


na katika utawa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.


Wapenzi, ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.


Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo