Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 11:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Fahamu, bassi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka ukali, bali kwako wema, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Ona, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Ona, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Ona, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Angalia basi wema na ukali wa Mungu: Ukali kwa wale walioanguka, bali wema wa Mungu kwako wewe, kama utadumu katika wema wake. La sivyo, nawe utakatiliwa mbali.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Angalia basi wema na ukali wa Mungu: Kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, kama utadumu katika wema wake. La sivyo, nawe utakatiliwa mbali.

Tazama sura Nakili




Waroma 11:22
33 Marejeleo ya Msalaba  

Nazo penye udongo mwema, hawa ndio ambao kwamba kwa moyo mzuri na mwema hulisikia neno, wakalishika, wakazaa kwa saburi.


Kilia tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na killa lizaalo hulisafisha illi lizidi kuzaa.


Bassi Yesu akawaamhia Wayahudi wale waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mu wanafunzi wangu kweli kweli;


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


na kwa hiyo mnaokolewa, ikiwa mnayashika sana maneno niliyowakhuhirieni; isipokuwa mliamini burre.


Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia.


Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalimtuma mtu illi niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, wala taabu yetu isiwe haina faida.


Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana.


Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.


Bassi, kumbuka ulikoanguka, nkatubu, ukayatende matendo ya kwanza. Lakini, usipotenda hivyo, naja kwako upesi, nitaondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo