Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 11:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, nauliza. Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! maana mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benjamin.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Basi, nauliza: Je, Mungu amewakataa watu wake? Hata kidogo! Mimi binafsi ni Mwisraeli, mzawa wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Basi, nauliza: Je, Mungu amewakataa watu wake? Hata kidogo! Mimi binafsi ni Mwisraeli, mzawa wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Basi, nauliza: je, Mungu amewakataa watu wake? Hata kidogo! Mimi binafsi ni Mwisraeli, mzawa wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi nauliza: Je, Mungu amewakataa watu wake? La, hasha! Mimi mwenyewe ni Mwisraeli, tena uzao wa Ibrahimu kutoka kabila la Benyamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi nauliza: Je, Mungu amewakataa watu wake? La, hasha! Mimi mwenyewe ni Mwisraeli, tena uzao wa Ibrahimu kutoka kabila la Benyamini.

Tazama sura Nakili




Waroma 11:1
17 Marejeleo ya Msalaba  

Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.


Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, nikalelewa katika niji huu miguumi pa Gamaliel, nikafundishwa sharia ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa ijtihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi:


Kwa maana Wayahudi wote wanajua maisha yangu tangu ujana, yaliyokuwa tangu mwanzo katika taifa langu Yerusalemi,


Bassi nasema, Je! wamejikwaa hatta wameanguka kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokofu umewafikilia mataifa, illi wao watiwe wivu:


Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na killa mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Illi upewe haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.


Kwa maana naliomba mimi mwenyewe niharamishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;


Wao Waebrania? Na mimi. Wao Waisraeli? Na mimi. Wao uzao wa Ibrahimu? Na mimi.


Nalitabiriwa siku ya nane, ni lutu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benjamin, Mwebrania wa Waebrania, kwa khabari ya kuifuata sharia, Farisayo, kwa khabari ya wivu, mwenye kuliudhi Kanisa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo