Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 10:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Lakini nasema, Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imetoka ikaenea katika inchi yote, Na maneno yao hatta miisho ya ulimwengu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Lakini nauliza: Je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Lakini nauliza: Je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Lakini nauliza: je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana: “Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana: “Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu.”

Tazama sura Nakili




Waroma 10:18
23 Marejeleo ya Msalaba  

Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.


Amin, nawaambieni, Killa ikhuhiriwapo injili hii katika ulimwengu wote, na hilo alilolitenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.


Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Tena Shetani akamchukua hatta mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fakhari yake, akamwambia,


Akawaambia, Enendem nlimwenguni mwote, mkaikhubiri injili kwa killa kiumbe.


Nao wakatoka, wakakhubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithubutishia neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Amin.


Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi.


hali kwanza niliwakhubiri wale wa Dameski na Yerusalemi, na katika inchi yote ya Yahudi, na watu wa mataifa, watubu wakamwelekee Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inakhubiriwa katika dunia yote.


katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


Maana kutoka kwenu Neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu: bali na katika killa mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea, hatta hatuna haja sisi kunena lo lote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo