Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 10:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Lakini wote hawakuipokea hiyo habari njema. Maana Isaya alisema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Lakini wote hawakuipokea hiyo habari njema. Maana Isaya alisema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Lakini wote hawakuipokea hiyo habari njema. Maana Isaya alisema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Lakini si wote waliotii Injili. Kwa maana Isaya asema, “Mwenyezi Mungu, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, “Bwana Mwenyezi, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”

Tazama sura Nakili




Waroma 10:16
21 Marejeleo ya Msalaba  

Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likinena, Kusikia mtasikia, wala hamtafahamu; Mkitazama mtatazama, wala hamtaona:


Lakini ninyi hamwamini kwa sababu hammo katika kondoo zangu, kama nilivyowaambieni.


Wengine waliamini yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini.


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


Lakini iwapo matawi mengine yamekatiwa, na wewe mzeituni mwitu ulitiwa kati yao ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,


ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;


na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, hasira na ghadhabu;


Ni nini, bassi, ikiwa hawakuamini wengine? Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?


Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;


ENYI Wagalatia msio akili, ni nani aliyewaloga, msiisadiki kweli, ninyi ambao Kristo aliwekwa mbele ya macho yemi ya kuwa amesulibiwa?


Mlikuwa mkipiga mbio vizuri: ni nani aliyewazuia msiitii kweli?


katika mwako wa moto, akiwalipa kisasi wao wasiomjua Mungu, nao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, akatoka aende hatta mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.


Maana ni kweli, sisi nasi tumekhubiriwa khabari njema kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa bao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


tena, Jiwe lakujikwaza mguu, na mwamba wa kujiangusha; maana hujikwaza kwa neno lile, wakiliasi, nao waliwekwa wapate hayo.


KADHALIKA ninyi wake, watumikieni waume o zenu; kusudi, ikiwa wako waume wasioliamini Neno, kwa mwenendo wa wake zao, pasipo Neno lile, wavutwe;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo