Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 1:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekima tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, yanafahamika kwa viumbe vyake, yaani uweza wake wa milele na Uungu wake; wtisiwe na udhuru:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uweza wake wa milele na asili yake ya uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.

Tazama sura Nakili




Waroma 1:20
37 Marejeleo ya Msalaba  

illi mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni: maana yeye jua lake huwazushia waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.


Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, Mungu aliwafanya mtu mume na mtu mke.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; sasa hawana udhuru kwa dhamhi yao.


Bassi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wana Adamu.


ENYI wanaume, ndugu zangu ua baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea nafsi yangu mbele yemi sasa.


Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana ni dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.


ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;


KWA hiyo, ee mtu uhukumuye uwae yote, huna udhuru; kwa maana katika hayo uhukumuyo mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.


hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na wakishitakiana killa mtu mwenzake kwa fikara zao na kuteteana;


Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mleta hoja wa dunia bii? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia liii kuwa upumbavu?


nae ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.


Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa namna ya kimwili.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


Kwa imani akatoka Misri, asiogope hasira ya mfalme; maana alistahimili kama amwonae yeye asiyeonekana.


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo