Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 1:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapeni karama ya rohoni, illi mfanywe imara;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kwa maana ninatamani sana kuwaoneni ili nipate kuwagawieni zawadi ya kiroho na kuwaimarisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kwa maana ninatamani sana kuwaoneni ili nipate kuwagawieni zawadi ya kiroho na kuwaimarisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kwa maana ninatamani sana kuwaoneni ili nipate kuwagawieni zawadi ya kiroho na kuwaimarisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ninatamani sana kuwaona ili nipate kuwapa karama za rohoni ili mwe imara,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ninatamani sana kuwaona ili nipate kuweka juu yenu karama za rohoni ili mwe imara,

Tazama sura Nakili




Waroma 1:11
32 Marejeleo ya Msalaba  

Makanisa yakatiwa nguvu kwa imani, hesabu yao ikaongezeka killa siku.


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


Na Paolo, alipokwisba kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.


yaani, tufarijiane mimi na ninyi, killa mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.


Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena tangu miaka mengi nikiwa na shauku kuja kwenu;


Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa haraka ya Injili ya Kristo.


nipate kufika kwenu kwa furaha, kama Mungu akipenda, nikapate kupumzika pamoja nanyi.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


Na nikiwa na timiaini hilo nalitaka kwenda kwenu hapo kwanza, illi mpate karama ya pili;


Bassi Yeye atufanyae imara pamoja na ninyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,


Maana yeye ajae akikhubiri Yesu mwingine ambae sisi hatukumkhubiri, au mkipokea Roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumilia nae.


Nao wenyewe, wakiwaombea ninyi, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sanu ndani yenu.


Maana Mungu ni shahidi wangu, jinsi ninavyowaonea shauku katika moyo wake Kristo Yesu.


Kwa kuwa alikuwa na shanku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi.


BASSI, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema.


Lakini Bwana ni mwaminifu, atakaewafanyeni imara na kuwaokoeni na yule mwovu.


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikieni kwa maneno machache, nikionya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli va Mungu. Simameni imara katika hiyo.


Kwa hiyo sitakosa kuwakumbusheni hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthubutishwa katika kweli iliyowatikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo