Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 4:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 4:6
33 Marejeleo ya Msalaba  

Ninyi ni chumvi ya dunia: lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwani ikolee? Haifai tena kabisa, illa kufupwa nje na kukanyagwa na watu.


Chumvi ni njema; lakini chumvi ikitokwa na ladhdha yake, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.


Wakamshuhudia wote, wakayastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake: wakanena, Huyu siye Mwana wa Yusuf?


Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, liwape neema wanaosikia.


Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.


bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu; mwe tayari siku zote kumjibu killa mtu akuulizae khabari za tumaini lililo ndani yenu; kwa upole na kwa khofu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo