Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 4:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 mkituombea na sisi pia, Mungu atufungulie mlango kwa Neno lake tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena neno lake, ili tupate kuitangaza siri ya Al-Masihi, ambayo kwa ajili yake nimefungwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Pia tuombeeni na sisi ili Mwenyezi Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Al-Masihi, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 4:3
27 Marejeleo ya Msalaba  

Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa.


Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wengi wako wanipingao.


MTU na atubesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.


Bassi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo nikafunguliwa mlango katika Bwana,


KWA sababu biyo mimi Paolo, mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa,—


ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri ile, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache,


kwa hayo, myasomapo, mtaweza kutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo;


na kuwaangaza watu wote, wajue khabari ya kuishiriki siri ile, ambayo tangu zamani zote ilisetirika katika Mungu, aliyeviumba vyote kwa Yesu Kristo:


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokofu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho ya Yesu Kristo,


kama ilivyo wajib wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kuitetea Injili na kuithubutisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii.


siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake:


Salamu yangu mimi Paolo, kwa mkono wangu mwenyewe. Yakumbukeni mafungo yangu. Neema na iwe pamoja nanyi. Amin.


Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu;


Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa: maana nataraja ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo