Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 4:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimuni. Daima anawaombeeni nyinyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimuni. Daima anawaombeeni nyinyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimuni. Daima anawaombeeni nyinyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Al-Masihi Isa, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Al-Masihi Isa, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mwenyezi Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 4:12
30 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


KWA kuwa wiitu wengi wametia mkono kutunga khabari za mambo yale yaliyotimizwa kati yetu,


Nae kwa kuwa alikuwa na huzuni sana, akazidi kuomba kwa bidii. Hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka hatta inchi.


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Na mimi mwenyewe, ndugu zangu, nimehakikishwa kwa khahari zenu kama ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.


Nakusihini, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami kwa maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu,


Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.


Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa;


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


Vitoto vyangu, ambao nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.


katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,


ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;


nami najitaabisha kwa hiyo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendae kazi ndani yangu kwa nguvu.


kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


pamoja ua Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu; watawaarifuni mambo yote ya huku.


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


Epafra, aliyefuugwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu;


Lakini chakula kigumu in cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.


Yeye siku hizo za niwili wake alimtolea yeye awezae kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa sababu ya kicho chake;


YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,


Na saburi iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa neno.


Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo