Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 4:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Na Yesu aitwae Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Isa aitwaye Yusto pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Isa, yeye aitwaye Yusto, pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 4:11
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.


Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi, wale walio wa Tohara wakashindana nae, wakisema,


Nisalimieni Priska na Akula, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,


na baba ya kutahiriwa, si kwa hao waliotahiriwa tu, bali kwa hao waliotahiriwa na kuzifuasa uyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa.


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


Kwa ajili ya hayo kumbukeni kwamba zamani, ninyi mlio watu wa mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa jina lenu wasiotahiriwra na wale wanaoitwa jina lao waliotahiriwa, yaani tohara ya mwili kwa mikono:


Naam, nakutaka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi nae, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.


Tukiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


kwa sababu hiyo tulifarijiwa, ndugu, kwa khabari zenu, katika shidda na mateso yetu yote, kwa imani yenu.


Maana wako wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo maana, wadanganyaji, khassa wale waliotahiriwa,


PAOLO, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yelu, kwa Filemon mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi,


na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo