Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 3:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Msiambiane uwongo, kwa kuwa mmemvua mtu wa kale, pamoja na matendo yake,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake,

Tazama sura Nakili




Wakolosai 3:9
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


tukijua haya, ya kuwa mtu wetu wa kale alisulibishwa pamoja nae, illi mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;


mvue kwa khabari ya desturi za kwanza mtu wa zamani, anaeharibiwa kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;


Bassi uvueni uwongo, mkaseme kweli killa mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, killa mmoja kiungo cha wenzake.


Lakini sasa yawekeni mbali haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.


na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na wawongo, mi waapao uwongo, na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;


Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyae machukizo na uwongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo