Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 3:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Yeyote atendaye mabaya atapewa adhabu ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Yeyote atendaye mabaya atalipwa kwa ajili ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 3:25
22 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Wakamwuliza, wakinena, Mwalimu, twajua ya kuwa wanena yaliyo kweli na kuyafundisha, wala hujali cheo cha mtu, bali katika kweli waifundisha njia ya Mungu:


Petro akafumhua kiuywa chake, akasema, Hakika nimekwisha kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;


kwa maana hapana upendeleo kwa Mungu.


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya.


mkijua ya kuwa killa neno jema atendalo mtu, atapewa lilo hilo na Bwana, akiwa ni mtumwa, au akiwa ni huru.


Na ninyi, akina bwana, watendeni yayo bayo, mkiacha kuwaogofya, mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, na kwake hapana upendeleo.


NINYI bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.


mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana.


kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi,


Na kama amekudhulumu, au awiwa nawe kitu, ukiandike juu yangu.


Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na killa kosa na uasi ulipata ujira wa haki,


Na ikiwa mnamwita Baba yeye ahukumuye killa mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa khofu kafika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni;


Watu hawa ni wenye kunungʼunika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno ya kiburi makuu mno, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo