Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 3:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana njira wa urithi; kwa kuwa mnamtumikia Bwana Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Isa Al-Masihi mnayemtumikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Isa Al-Masihi mnayemtumikia.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 3:24
31 Marejeleo ya Msalaba  

Ampokeae nabii kwa kuwa yu nabii, atapata thawabu ya nabii; nae ampokeae mwenye haki kwa kuwa yu mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.


Furahini, shangilieni: kwakuwa thawabu yenu nyingi mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.


Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo?


Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.


Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


kwa sababu hawana kitu cha kukulipa; maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.


Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu.


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,


Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo haya humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wana Adamu.


Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowakhubirini, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,


Bassi yeye apandae, na yeye atiae maji ni kitu kimoja, na killa mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.


Kwa maana yeye aliyekwitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye nae aliyekwitwa hali ya uhuru, ni mtuniwa wa Kristo.


Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


wala si kwa utumwa wa macho kama wajipendekezao kwa wana Adamu; bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;


mkijua ya kuwa killa neno jema atendalo mtu, atapewa lilo hilo na Bwana, akiwa ni mtumwa, au akiwa ni huru.


Mtu asiwanyangʼanye thawabu yenu, akijinyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kwa kuwaabudu malaika, akijishughulisha na asiyoyaona, akijivuna burre, kwa akili ya mwili wake,


Bassi msiutupe njasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.


Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.


Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.


tupate urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu,


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo