Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 3:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wana Adamu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo wote kama watu wanaomtumikia Bwana Isa, na si wanadamu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana Isa, na si wanadamu,

Tazama sura Nakili




Wakolosai 3:23
18 Marejeleo ya Msalaba  

Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.


Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.


Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Bassi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.


Ninyi wake, watumikieni waume zenu kama kumtumikia Bwana wetu.


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Tumikieni killa kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa mfalme, kama mwenye cheo kikuliwa;


kwa sababu ndio mapenzi ya Mungu, kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo