Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 3:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Ninyi watumwa, watiini wao ambao kwa niwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wana Adamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimeha Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kujipendekeza tu kwao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana Isa.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 3:22
22 Marejeleo ya Msalaba  

Taa ya mwili ni jicho; bassi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.


Maana na mimi ni mtu chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; au mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.


Ya nini kuniita Bwana, Bwana, nanyi hamyatendi niyanenayo?


Sababu mimi nami ni mtu aliyewekwa chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda: na huyu, Njoo, huja; na mtumishi wangu, Fanya hivi, hufanya.


Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jamlio hili lapendeza katika Bwana.


bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuaminiwe Injili ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wana Adamu bali Mungu anaetupima mioyo yetu.


tokea sasa, si kama mtumwa, baii lieha ya mtumwa, ndugu mpendwa, kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo