Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 2:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 mmetia mizizi, na kujengwa katika yeye: mmefanywa imara kwa imani, kaina mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Muwe na mizizi ndani yake, mjijenge juu yake na kuwa imara katika imani kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Muwe na mizizi ndani yake, mjijenge juu yake na kuwa imara katika imani kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Muwe na mizizi ndani yake, mjijenge juu yake na kuwa imara katika imani kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 mkijikita na kujengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa, na kufurika kwa wingi wa shukrani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 mkiwa na mizizi, na mmejengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa, na kufurika kwa wingi wa shukrani.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 2:7
31 Marejeleo ya Msalaba  

Mfano wake ni mtu ajengae nyumba, akafukua, akachimba chini sana, akaweka msingi wake juu ya mwamba. Bassi palipokuwa na gharika, mto ukairukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa, kwa kuwa msingi wake umewekwa juu ya mwamba.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


na yeye atawathubutisheni hatta mwisho, msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


Bassi Yeye atufanyae imara pamoja na ninyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,


Kristo akae mioyoni mwemi kwa imani; illi ninyi, mkiwa na mizizi na misingi katika upendo,


mkiwa mwalimsikia mkafundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli katika Yesu;


mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


shukuruni kwa killa jambo; maana haya ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.


awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema.


Bassi na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo ya watu waliungamao jina lake.


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Watu hawa ni miamba yenye khatari katika karamu zenu za upendo wafanyapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo khofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa marra mbili, na kungʼolewa kabisa;


Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imaui yenu iliyo takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu,


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo