Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 2:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 illi wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Nafanya hivi kusudi mioyo yao ifarijiwe na kuvutwa pamoja katika upendo, ili wajazwe uthabiti mwingi uletwao na elimu ya kweli. Hapo wataijua siri ya Mungu ambayo ni Kristo mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Nafanya hivi kusudi mioyo yao ifarijiwe na kuvutwa pamoja katika upendo, ili wajazwe uthabiti mwingi uletwao na elimu ya kweli. Hapo wataijua siri ya Mungu ambayo ni Kristo mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Nafanya hivi kusudi mioyo yao ifarijiwe na kuvutwa pamoja katika upendo, ili wajazwe uthabiti mwingi uletwao na elimu ya kweli. Hapo wataijua siri ya Mungu ambayo ni Kristo mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Kusudi langu ni watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu mkamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani Al-Masihi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Kusudi langu ni watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu mkamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani, Al-Masihi mwenyewe,

Tazama sura Nakili




Wakolosai 2:2
58 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.


Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa.


KWA kuwa wiitu wengi wametia mkono kutunga khabari za mambo yale yaliyotimizwa kati yetu,


Mimi na Baba yangu tu nmoja.


lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi, mpate kujua na kuamini ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.


Yote aliyo nayo Baba m yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Yesu akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hatta sasa, nami ninatenda kazi.


illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka.


Nasi tumeamini, tena tumejua ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Na jamii ya watu walioamini walikuwa moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


Au waudharau wingi wa wema wake na uvumilivu wake na kusubiri kwake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvutia toba?


Kwa maana nyote mwaweza kukhutubu mmoja mmoja, illi wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.


Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;


awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho yake, katika mtu wa ndani;


ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri ile, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache,


ambae nilimpeleka kwenu kwa kusudi hili hili mpate kuyajua mambo yetu, nae akawafariji mioyo yenu.


BASSI ikiwako faraja iliyo yote katika Kristo, yakiwako ma, tulizo yo yote ya mapenzi, ikiwako huruma yo yote na rehema,


Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo;


siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake:


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


wala hakishiki kiehwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua mkuo utokao kwa Mungu.


Juu ya haya yote vaeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.


mkituombea na sisi pia, Mungu atufungulie mlango kwa Neno lake tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,


ambae nimemtuma kwenu kwa sababu hiyo hiyo, ajue mambo yenu, akawafariji mioyo yenu;


kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthubutifu mwingi; kama mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.


Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho;


Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.


kwa kuwa uweza wa Mungu umetukarimia vitu vyote vyenye uzima na utawa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe;


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Hivi tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, na mbele zake tutatuliza mioyo yetu


Kwa maana watatu ni mashahidi mbinguni, Baba, Neno, na Robo Mtakatifu, ua watatu hawa ni umoja.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo