Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 2:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Mtu asiwanyangʼanye thawabu yenu, akijinyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kwa kuwaabudu malaika, akijishughulisha na asiyoyaona, akijivuna burre, kwa akili ya mwili wake,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira danganyifu za kidunia

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira danganyifu za kidunia

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira danganyifu za kidunia

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Mtu yeyote asiwaondolee thawabu yenu kwa kusisitiza unyenyekevu wa uongo na kuabudu malaika. Mtu kama huyo hudumu katika maono yake, akijivuna bila sababu katika mawazo ya kibinadamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Mtu yeyote asiwaondolee thawabu yenu kwa kusisitiza unyenyekevu wa uongo na kuabudu malaika. Mtu kama huyo hudumu katika maono yake, akijivuna bila sababu katika mawazo ya kibinadamu.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 2:18
42 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kwa uwongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anaehimidiwa milele. Amin.


Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.


Upendo husubiri, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni,


Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu.


Wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu.


Mambo haya, ndugu, nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na wa Apollo kwa ajili yemi, illi kwa khabari zetu mpate kujifunza katika fikara zenu kutokuruka mpaka wa yale yaliyoandikwa; mtu mmoja asijivune juu ya mwenziwe, kwa ajili ya mtu mwingine.


NA kwa khabari ya vitu, vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna elimu. Elimu huleta majivuno, bali upendo hujenga.


Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.


Lakini naogopa; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikara zenu, mkauacha unyofu wenu kwa Kristo.


Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;


Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,


Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo maana; maana kwa sababu ya haya ghadhabu ya Mungu huwajia wana wa uasi.


nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.


Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kujinyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali: illakini hayafai kitu wala kuwa dawa ya tamaa za mwili.


Nasema neno hili, mtu asije akawadanganyeni kwa maneno yaliyotungwa illi kuwakosesha.


Angalieni intu asiwateke kwa filosofia yake na madanganya matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wana Adamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.


wapenda kuwa waalimu wa sharia, wasiyafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa utbabiti.


ROHO yanena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho watu watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani,


wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kukhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo ilivozoezwa kutamani, wana wa laana;


Nimewaandikia haya katika khabari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo