Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 2:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Bassi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au viuvwaji au kwa sababu ya siku kuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au Sabato.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au Sabato.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au Sabato.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi kuhusu vyakula au vinywaji, au kuhusu kuadhimisha sikukuu za dini, au Sikukuu za Mwezi Mwandamo au siku ya Sabato.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kwa hiyo mtu asiwahukumu ninyi kuhusu vyakula au vinywaji, au kuhusu kuadhimisha sikukuu za dini, au Sikukuu za Mwezi Mwandamo au siku ya Sabato.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 2:16
42 Marejeleo ya Msalaba  

Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho najis mwana Adamu; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho najis mwana Adamu.


kwa sababu hakimwingii moyoni, illa tumboni tu; kiisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.


balituwaandikie wajiepushe na unajisi wa sanamu na asharati na nyama zilizosongwa na damu.


Lakini wewe je! mbona wamhukumu ndugu yako? na wewe je! mbona wamdbarau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.


Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.


Bassi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkaacha mafundisho ya awali ya ulimwengu, ya nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


kwa kuwa ni sharia za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hatta wakati wa matengenezo mapya.


Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo