Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 2:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 akiisha kuziteka enzi na mamlaka, na kuzimithilisha kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Baada ya Mungu kuzivua enzi na mamlaka, aliziaibisha hadharani, akishangilia katika ushindi wa msalaba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Mungu akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuziburura kwa ujasiri, akizishinda katika msalaba wa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 2:15
25 Marejeleo ya Msalaba  

Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? ndipo atakapoiteka nyumba yake.


Akawaambia, Nalimwona Shetani kama umeme akianguka toka mbinguni.


lakini mwenye nguvu za kumpita yeye atakapokuja na kumshinda, amnyangʼanya silaha zake zote alizotegemea, na mateka yake ayagawanya.


kwa khabari ya hukumu, kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amehukumiwa.


Bassi Yesu alipoipokea siki, akasema, Imekwisha: akainama kichwa, akatoa roho.


Ndipo palipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.


Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


illi sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka ya mbinguni;


Kwa biyo asema, Alipopanda juu, aliteka mateka, Akawapa watu vipawa.


Kwa maana shindano letu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza ya ulimwengu huu, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.


Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya inchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake,


Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi vote na mamlaka.


Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo