Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 1:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 tuliposikia khabari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Maana tumesikia juu ya imani yenu kwa Kristo Yesu na juu ya mapendo yenu kwa watu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Maana tumesikia juu ya imani yenu kwa Kristo Yesu na juu ya mapendo yenu kwa watu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Maana tumesikia juu ya imani yenu kwa Kristo Yesu na juu ya mapendo yenu kwa watu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Al-Masihi Isa, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Al-Masihi Isa, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote:

Tazama sura Nakili




Wakolosai 1:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

Wala si kwa kuwapo kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu khabari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hatta nikazidi kufurahi.


Maana ninyi nyote ni wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Kwa sababu hiyo na mimi, tangu nilipopata khabari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,


kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Lakini Timotheo alipotujia siku hizi kutoka kwenu, akatuletea khabari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote: mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi ninyi;


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


nikisikia khabari ya upendo wako na ya imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote;


maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.


Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mauti hatta uzima, kwa maana twawapenda ndugu. Asiyependa, akaa katika mauti.


Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri.


Na sisi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu ndani yetu na kuliamini. Mungu ni pendo, nae akaae katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo