Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 1:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote nae, akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya inchi, au vilivyo mbinguni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Kwake vitu vyote vilipatanishwa na Mungu: Na kwa damu yake msalabani akafanya amani na vitu vyote duniani na mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Kwake vitu vyote vilipatanishwa na Mungu: Na kwa damu yake msalabani akafanya amani na vitu vyote duniani na mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Kwake vitu vyote vilipatanishwa na Mungu: na kwa damu yake msalabani akafanya amani na vitu vyote duniani na mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 na kupitia kwake aweze kuvipatanisha vitu vyote kwake mwenyewe, viwe ni vitu vilivyo duniani au vilivyo mbinguni, kwa kufanya amani kwa damu yake iliyomwagika msalabani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 na kwa njia yake aweze kuvipatanisha vitu vyote na yeye mwenyewe, viwe ni vitu vilivyo duniani au vilivyo mbinguni, kwa kufanya amani kwa damu yake, iliyomwagika msalabani.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 1:20
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atazaa mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, ndiye atakaewaokoa watu wake na dhambi zao.


Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.


Kornelio akanena, Leo ni siku ya nne tangu nilijiokuwa nikifunga hatta saa hii: na saa tissa nalikuwa nikisali nyumbani mwangu: kumbe! mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zingʼaazo, akasema,


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


ya kwamba wakati mkamilifu utakapowadia atajumlisha vitu vyote viwe umoja katika Kristo, vitu vilivyo mbinguni, navyo vilivyo duniani, katika yeye huyu:


illi kwa jina la Yesu killa goti likunjwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya inchi;


Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya inchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake,


Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo