Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wakolosai 1:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya inchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Maana kwake vitu vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: Wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu. Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Maana kwake vitu vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: Wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu. Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Maana kwake vitu vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu. Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kwake yeye vitu vyote vilivyo mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya utawala au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa kupitia kwake na kwa ajili yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kwake yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 1:16
29 Marejeleo ya Msalaba  

Alikuwako ulimwenguni, ulimwengu umepata kuwa kwa veye, wala ulimwengu haukumtambua.


Vyote vyalifanyika kwa huyu. Wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


Kwa maana tumekwisha kujua hakika ya kuwa hatta mauti haiwezi kututenga, wala nzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala wenye uwezo, wala yaliyopo, wala yatakayokuwa,


na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.


illakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu, aliye Baba, ambae vitu vyote vimetokana nae, na sisi twarejea kwake; na yuko Bwana mmoja Yesu Kristo, ambae kwa sabiki yake vitu vyote vimekuwa, na sisi kwa sabiki yake.


ya kwamba wakati mkamilifu utakapowadia atajumlisha vitu vyote viwe umoja katika Kristo, vitu vilivyo mbinguni, navyo vilivyo duniani, katika yeye huyu:


Kwa maana shindano letu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza ya ulimwengu huu, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.


illi kwa jina la Yesu killa goti likunjwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya inchi;


nae ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.


na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote nae, akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya inchi, au vilivyo mbinguni.


Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi vote na mamlaka.


akiisha kuziteka enzi na mamlaka, na kuzimithilisha kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.


mwisho wa siku bizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi yote, kwa yeye aliufanya ulimwengu.


Kwa kuwa ilimpasa veye, ambae kwa ajili yake na kwa kazi yake vitu vyote vimekuwa, akileta wana wengi hatta utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokofu wao kwa mateso.


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo