Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 4:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia, na kuyaona kwangu, yatendeni haya; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Tekelezeni yale mliyojifunza na kupokea kutoka kwangu; mambo mliyosikia nimesema na kuona nimeyatenda. Naye Mungu anayetujalia amani atakuwa pamoja nanyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Tekelezeni yale mliyojifunza na kupokea kutoka kwangu; mambo mliyosikia nimesema na kuona nimeyatenda. Naye Mungu anayetujalia amani atakuwa pamoja nanyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Tekelezeni yale mliyojifunza na kupokea kutoka kwangu; mambo mliyosikia nimesema na kuona nimeyatenda. Naye Mungu anayetujalia amani atakuwa pamoja nanyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 4:9
36 Marejeleo ya Msalaba  

Angalia, mwanamke bikira atachukua mimba, nae atazaa mwana, Na watamwita jina lake Immanuel; tafsiri yake, Mungu kati yetu.


mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.


Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.


Ya nini kuniita Bwana, Bwana, nanyi hamyatendi niyanenayo?


Lakini yeye akajibu akawaambia, Mama yangu na ndugu zangu ndio hawa walisikialo neno la Mungu na kulitenda.


Mkiyajua hayo, m kheri mkiyatenda.


Ninyi m rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.


Mama yake akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambieni fanyeni.


Lakini simama, uingie mjini, utaambiwa yatakayokupasa kutenda.


Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amin.


Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu kwa upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.


Bassi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.


Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.


Bassi, nawasihini, mwe wafuasi wangu.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Mwe wafuasi wangu, ndugu, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliokupeni.


Na amani va Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.


Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea Neno katika mateso mengi pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu,


Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi;


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tuliyowaagizeni, tena kwamba mtayafanya.


Bwana Yesu Kristo awe pamoja na roho yako. Neema na iwe nanyi. Amin.


Mwe watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, mkijidanganya nafsi zenu.


Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.


na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo